28 Januari 2026 - 13:34
Kumbukumbu ya Kuzaliwa kwa Imam Hussein (a.s)

Imam Hussein (a.s) anajulikana kwa kun'ya ya Abu ‘Abdillah, na miongoni mwa lakabu zake ni: As-Sayyid, Az-Zakiy, Al-Mubarak na As-Sibt. Mtume (s.a.w.w) alisema kuhusu yeye na kaka yake: “Wao ni mabwana wa vijana wa Peponi.”

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Baada ya kuzaliwa kwa Imam Hasan (a.s), Mtume Muhammad (s.a.w.w) alimfundisha binti yake Fatima (a.s) kuhusu malezi ya watoto wa Ahlul-Bayt kwa mapenzi na mpango wa Mwenyezi Mungu. Alipokuwa mjamzito wa Imam Hussein (a.s), Mtume (saww) alimwambia Fatima (sa) asimnyonyeshe mtoto huyo mpaka aje yeye mwenyewe, kwa kuwa Jibril (as) alimletea bishara ya kuzaliwa kwake.

Fatima (a.s) alijifungua Imam Hussein (a.s) wakati Mtume akiwa safarini, lakini hakumnyonyesha mpaka Mtume aliporejea. Mtume alipomchukua Hussein (as), aliweka ulimi wake kinywani mwa mtoto huyo, naye akaanza kunyonya. Mtume (saww) akasema kwa mapenzi: “Pole pole, Hussein… pole pole, Hussein.”

Kisha Mtume (s.a.w.w) akasema: “Allah anakataa isipokuwa Anachokitaka. Hiki kiko ndani yako na ndani ya kizazi chako,” akimaanisha kuwa ndani ya Imam Hussein (as) na vizazi vyake kuna Uimamu wa Kiungu.

Imam Hussein (a.s) anajulikana kwa kun'ya ya AbuAbdillah, na miongoni mwa lakabu zake ni: As-Sayyid, Az-Zakiy, Al-Mubarak na As-Sibt. Mtume (s.a.w.w) alisema kuhusu yeye na kaka yake: “Wao ni mabwana wa vijana wa Peponi.”

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha